Kwanini upakue app ya Kitengeneza Matusi Mabaya, ukilinganisha na app nyingine za matusi?

<b>Urahisi</b>
Muonekano wake ni rahisi kutumia, na matusi yote ni ya kiwango cha juu. App hii ilitengenezwa ili kukupa furaha unapoitumia.
Katika skrini kuu ya app, utakuwa na uwezo wa kutengeneza na kupitia matusi kadhaa mabaya. Kutumia app hii ni rahisi sana, na itakuchukua sekunde tu kutengeneza tusi jipya. Unaweza kuyapitia kwa urahisi kwa kugusa tu skrini yako.

<b> Ni Bure & Wazi</b>
App hii ni bure kabisa kuitumia na itabaki kuwa hivyo siku zote. Chanzo cha msimbo kinapatikana GitHub. Hauhitaji kuwa na hofu juu uanachama maalumu, malipo ya mwaka au gharama zilizofichwa ili kupata matokeo na kuwatumia wengine.

<b>Shirikisha wengine</b>
Tulijikita katika kurahisisha namna ya kutumia app hii. Utaweza kushirikisha wengine matusi yatakayotengenezwa na Evil Insult Generator bure. Matusi yako yanaweza kutumwa kwa wengine katika app mbalimbali. 

<b>Inarekebishwa Mara kwa mara</b>
Timu ambayo ilitengeneza app hii huwa wanaongeza matusi mara kwa mara. Ni rahisi kutuma kila tusi kwa wengine, na wengine wanaweza kulitumia, wakitaka. 
Lakini tunahitaji msaada wako. Tafadhali tutumie matusi yako na tutayapitia. Kama tukiyapenda, basi yatakuwepo katika toleo jipya la app. 

<b>Mkusanyiko Mkubwa wa Matusi</b>
App hii haikosi matusi ambayo unaweza kuyatumia. Matusi mengi kati ya haya ni ya kipekee na huwezi kuyapata mahali popote pengine.
Usichelewe - pakua app ya matusi mabaya na upate mistari ya kibunifu ambayo unaweza kuitumia kwa mtu yeyote!
Tuhajitahidi kuboresha ufanisi wa mtumiaji kwa kila mtu. Tunakaribisha maoni. Kama una mapendendekezo au ushauri, tungependa kuyasikia. Usisite kuwasiliana nasi kupitia marvin@evilinsult.com. Ukifanya hivyo, tutaweza kuboresha app na kuifanyia marekebisho na kuongeza matusi ya kisasa zaidi.

<b>ℹ️Kumbukaℹ️</b>
- Chanzo kinaweza kupatikana hapa: https://github.com/EvilInsultGenerator/android-app
- Tunashukuru sana kwa msaada wako katika kutafsiri app hii: https://crowdin.com/project/evil-insult-generator-android/
- Unakaribishwa sana kunitumia matusi yako pendwa ili niweze kuyaongeza

<b>⚠️Onyo⚠️</b>
Matusi mengi ambayo yametengenezwa na app hii yatawakasirisha baadhi ya watu, kwahiyo uwe makini unatumia matusi haya kwa nani. App hii ni kwa watu wenye umri mkubwa tu.
